KWA HILI LAZIMA MLIE NALO. PAGUMU HAPO!!
HAYA MABADILIKO YA UPINZANI BUNGENI NI KWA
SABABU YA NINI?
Mabadiliko haya ni
kwa sababu ya ZITTO tu au ni kwa sababu ya KASKAZINI??
- Panga pangua hiyo ambayo imesukumwa na kuvuliwa nyadhifa zote kwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe itawalenga pia mawaziri vivuli walioshindwa kutimiza majukumu yao kikamilifu au ni Zitto pekeyake?
Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, itafanya
mabadiliko makubwa katika Baraza lake Kivuli wakati wa Mkutano Mkuu wa 14 wa
Bunge ulioanza mapema mwezi huu mjini Dodoma. Panga pangua hiyo ambayo
imesukumwa na kuvuliwa nyadhifa zote kwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema
na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe itawalenga pia
mawaziri vivuli walioshindwa kutimiza majukumu yao kikamilifu.
Habari zilizopatikana jana mjini Dodoma
zilisema Zitto ni mlengwa mkuu wa mabadiliko hayo ikiwa ni utekelezaji wa
maazimio ya Kamati Kuu (CC) ya chama chake.
Kamati Kuu chini ya Mwenyekiti wake,
Freeman Mbowe iliagiza kuvuliwa nyadhifa zote, Zitto pamoja na Mjumbe wa Kamati
Kuu, Dk Kitilla Mkumbo kwa kile kilichodaiwa ni kukisaliti chama.
Kwa mujibu wa habari hizo, katika Mkutano
wa 14 wa Bunge ulioanza mapema mwezi huu, kambi rasmi ya upinzani imepanga
kumvua rasmi Zitto nafasi ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Waziri
Kivuli wa Fedha. Jana, Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu
alithibitisha kuwapo kwa mpango wa mabadiliko hayo na kwamba yanatarajiwa
kufanyika kati ya mwishoni mwa wiki hii na mwanzoni mwa wiki ijayo. “Tutakaa
mwishoni mwa wiki hii au mwanzoni mwa wiki ijayo kwa sababu Kiongozi wa Kambi
(Freeman Mbowe), atafika bungeni Desemba 6, mwaka huu na ndiye Mwenyekiti wa
Baraza Kivuli,” alisema Lissu na kuongeza:
“Mbali ya Zitto kuna Said Arfi (Mbunge
wa Mpanda Mjini) ambaye amejiuzulu nafasi zake zote ikiwa ni pamoja na Waziri
Kivuli wa Uchukuzi na tutaangalia ufanisi wa mawaziri wengine kivuli”.
Baraza kivuli linaundwa na mawaziri 18
wakiongozwa na Mbowe na Zitto aliyekuwa Naibu wake na Manaibu saba.
Kujitoa kwa wanachama
Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Iramba
Mashariki, alisema angeogopa kama kungekuwa na wimbi la wanachama zaidi ya
1,000 kuondoka katika chama kupinga misingi ya chama.
“Lakini kama walimfuata Zitto ndani ya
chama ni ruksa sisi hatuna shida lakini kama ni chama hapo kuna la kuangalia…
Sisi tunaamini wanachama wetu hawafuati mtu, bali misingi,” alisema.
SIKUZOTE KILA MUWAMBA NG’OMA LAZIMA AVUTIE KWAKE. YETU MACHO SISI.
TUNARUDI KULE
KULE“ WANAJUA MBIO TUNAZIJUA NJIA’’ Hata siku moja siasa haitafanyika kwa misingi ya UKABILA na UDINI.
0 comments:
Post a Comment