NEWZZZZ...........

THE VOICE OF UVCCM ILEMELA MWANZA
MWENYEKITI WA UVCCM ILEMELA COMRED KHERI .D. JAMES

UFISADI MTUPU HUU!!!!



UFISADI MTUPU HUU!!!!
Leo kumesambaa taarifa ya kukamatwa gari ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe,Mwenyekiti wa CDM na Mbunmge wa jimbo la Hai.
Gari hiyo ni kwa shughuli za bunge tu na linapotumika lazima kuwe na taarifa rasmi toka kwa Uongozi wa Buneg chini ya Katibu wake Dk Thomas Kashilillah.
Bahati mbaya iiliyoje ni kwamba Mhe Mbowe licha ya kuwa na magari kadhaa ya kichama na ya kibinafsi lakini amekuwa ni mfujaji wa mali za umma kwa kulitumia gari hilo kwa shughuli zake binafsi.
Hivi kweli inaingia akilini kwa Mhe Mbowe na mwenzake Mhe Wenje kutoka Dar es Salaam na gari hilo aina ya VX V8 land Cruiser kwenda Mombasa kutembea kwa maswala yao binafsi kisha kumwacha Driver Ndg Ibrahim hotelini na wao kupanda ndege kwenda Nairobi wakitokea Mombasa?
Kwa nini wasiwe na uchungu na fedha za walipa kodi wa nchi hii?
Umbali wa Mombasa via Voi -Tsavo West mpaka Nairobi ni takriban kilometa 470 (umbali wa Dar -Dodoma) huku barabara ikiwa na lami tupu na usalama wa kutosha karibu kila miji iliyopo baina ya miji mikubwa hiyo.
Kama watu walitoka Dar kwa gari hilo na kutumia fedha za serikali kama mafuta na posho ya dereva kisha kufika Mombasa wamwache dereva huyo je kuna umuhim gani kwa viongozi hao kutumia ndege toka Mombasa-Nairobi?huu ni ufisadi na ufujaji wa hali ya juu wa fedha na naomba Mhe Mbowe na mwenzake waombe radhi kwa hilo maana wameitia hasara nchi,hata kama ni kidogo lakini kinapaswa kuheshimiwa!
Inashangaza sana mtu kutumia mamilioni ya fedha za mafuta kisha kufika huko na wakaamua kulitekeleza gari hilo hotelini huku wao wakiruka?
HUU NI UFISADI UNAOPASWA KUPINGWA KWA NGUVU ZOTE BILA YA KUJALI ITIKADI ZA VYAMA.
Pia tunataka kujua kisa cha kutumia gari hiyo kwa namba mbili inapokuwa nje ya nchi maana huu nao ni mmojawapo wa mpango wa ugaidi.Huwezi kuvuka katika mpaka wa nchi yoyote huku ukitumia namba za gari tofauti kama upo ndani ya nchi husika.Kenya ni nchi huru na yenye sheria zake zinazopaswa kuheshimiwa na watu jamii kama ya akina Mhe Mbowe na Mhe Wenje.
Hivi walivyofika mpakani kwa upande wa Kenya (Lungalunga) walikuwa wakitumia namba gani?na je hawakugundua kuwa wanapaswa kuwa na namba moja ianyotambulika?
Hili lazima tulikemee na kulipinga kwa nguvu zote kwa KUSEMA NO KWA MHE MBOWE NA MHE WENJE MAANA WAMELITIA DOA TAIFA LETU KWA GARI LAKE KUONEKANA NI SEHEMU YA SHAKA LA UGAIDI NDANI YA NCHI NYINGINE.  


0 comments: