HONGERA DR. ASHA-ROSE MIGIRO. M/KITI WETU TAIFA AMEKUAMINI NA SISI PIA TUNAKUAMINI
(NAPE NNAUYE AKIMPONGEZA DR. ASHA-ROSE MIGIRO
BAADA YA KUTEULIWA KUWA MBUNGE.)
Naibu
katibu mkuu mstaafu wa umoja wa mataifa
na pia ni katibu wa halmashauri kuu ya chama cha
mapinduzi (NEC) siasa na kimataifa Dr. Asha-Rose Migiro.
Jana aliteuliwa rasmi na raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania amabae pia
ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi
taifa Dr. Jakaya Kikwete kuwa mbunge wa bunge la jamuhuri ya muungano wa
Tanzania anaeteuliwa na raisi. Kwamujibu wa katiba ya jamuhuri ya muungano wa
Tanzania, raisi anamamlaka ya kuteua wabunge kumi na kuwafanya kuwa miungoni
mwa wabunge wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Kwa kufanya
hivyo Mh. Kikwete ameonyesha jinsi gani
alivyomuamini na kuukubali utendaji na uwajibikaji wa Dr. Asha-Rose Migiro
tangu alipo kuwa akifanya kazi za umoja wa mataifa(UN). Lakini pia Mh. Raisi ameonyesha jinsi
gani anavyo waamini akina mama wote wa Tanzania pamoja na mchango wao katika
jamii na maendeleo ya nchi yetu.
Umoja
wa vijana wa chama cha mapinduzi
wilaya ya Ilemela na mkoa wa Mwanza kwa ujumla unampongeza Dr. Migiro kwa
kuaminiwa na Mh. Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kuwa miungoni mwa
wabunge wa bunge letu la Tanzania. Chama cha
mapinduzi ni chama cha watu wa aina zote, wanaume kwa wanawake,
vijana kwa wazee na pia ni chama cha makabila na dini aina zote. Kidumu chama cha
mapinduziiiiii, Kidumu chama tawalaaa!!!!
0 comments:
Post a Comment