SERIKALI YABARIKI UCHAGUZI WA MEYA NA NAIBU MEYA ILEMELA. WAZIRI GHASIA AFAFANUA. WASHINDANI WANYAMAZISHWA.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi). Hawa
Ghasia amethibitisha kuwa uchaguzi huo wa Meya na Naibu meya wa wilaya ya Ilemela
ulikuwa wa haki na akidi ilikamilika. Ghasia alikuwa akijibu swali la nyongeza
la Mbunge wa Nyamagana Hezekiah Wenje juzi bungeni aliyetaka serikali kutoa
tamko la kufuta uchaguzi huo. Hata hivyo Waziri Ghasia aliendelea na msimamo wake
kwamba akidi katika uchaguzi huo ilitimia hivyo viongozi waliochaguliwa ni
halali. Licha ya kuwa uchaguzi huo
ulihudhuriwa na madiwani 6 kati ya 14, lakini bado ni halali kutokana na
wajumbe 3 wa baraza la madiwani kufungiwa kwa muda wa miezi 3 kwa kosa la kudharau
amri halali ya mahakama na wengine 5
kugoma kuhudhuria mkutano huo pamoja na kupatiwa taarifa na Mkurugenzi. ‘‘Wajumbe
6 walifanya uchaguzi huo ni halali kwa kuwa ulihudhuriwa na zaidi ya nusu ya
wajumbe halali walio paswa kuhudhuria kikao hicho ambao walitakiwa kuwa 11’’
aliseama Waziri Hawa Ghasia. Kwamujibu wa maelezo ya Waziri Hawa Ghasia Meya wa
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mh. Henry Matata na Naibu Meya Mh. Swila Dede
Swila wapo kihalali na hakuna utata tena juu ya hilo.
0 comments:
Post a Comment