KIGOMA YAONYESHA HATIMA YA CHADEMA. KATIBU MKUU SLAA APOKELEWA NA WATU WACHACHE HASA WATOTO.
Kwakweli kila lenye mwazo halikosi
kuwa na mwisho. Kipimo kikuu cha maendeleo huwa ni kutoka 0-1000 nasio 100-10.
Hii ni hesabu rahisi sana kwa watu wenye busara na hekima lakini kwa watu walio
na upeo mdogo wakuelewa kamwe hawatanielewa nini kinamaanishwa hapa. Mwanzoni
walipo kuwa wakiitisha mikutano watu wengi walijitokeza kutaka kuwasikiliza
mamia kwa maelfu wazee kwa vijana, waume kwa wanawake, watoto kwa wakubwa wote
walikua wakikusanyika kwa pamoja katika
viwanja husika. Leo mambo yameanza kubadilika, mahudhurio kwa wafuasi yameshuka
kwa kasi ndani ya mda mfupi sana hasa baada ya kumvua uongozi alie kuwa naibu
katibu mkuu wa CHADEMA taifa Zitto Kabwe. Hii inaonyesha ni jinsi gani chama kilivyo
mikononi mwa watu nasio mioyoni mwa watu. Kiukweli hali ya hewa sio nzuri kwa
ndugu zetu ila wanajikaza tu ili kuficha aibu yao. Hata siku moja huwezi
kumfukuza mtu katika nafasi furani tena kwa vitisho alafu baadae urudi kwenye
jimbo lake au kwa wapiga kula wake ili kuzidi kumchafua halafu wakusikilize
wakati wao hawaoni kosa. Wakikuheshimu sana wataondoka wala hawata kuja
kukusikiliza kamwe na ukizidi kuwasumbua watakupiga. Hivi ndivyo ilivyokuwa
mkoa wa Kigoma siku chache zilizopita wakati katibu mkuu wa CHADEMA Dr.Slaa alipoenda
kuzulu katika mkoa huo na kupokelewa na watu wachache hasa wengi wao wakiwa watoto
kama picha inavyo honyesha na si vinginevyo. Katibu mkuu huyo alizidi kuwakera
watu zaidi pale aliposema wanaomlilia Zitto waondoke naye. Haya hayakuwa maneno
mazuri sana ya kuongea mbele ya wapiga kula na wana chama wa mbunge husika.
Kweli hali hii sio nzuri.
0 comments:
Post a Comment