HOTUBA YA RAISI KIKWETE NCHINI A.KUSINI KATIKA MAZISHI YA MADIBA IMETUNG'ARISHA WATANZANIA. WASOUTH WATOKWA MACHOZI YA FURAHA.
Hotuba ya Raisi wa Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete imezidi kujenga na kuimarisha
uhusiano wa Tanzania na Afrika kusini. Kupitia hotuba yake nzuri Raisi Kikwete
ameeleza kwa undani zaidi jinsi nchi ya Tanzania ilivyo husika kwa sehemu kubwa
kuhakikisha Afrikakusini inapata demokrasia ya kweli na kuondoa ubaguzi wa
rangi uliokuwa umeshamiri katika nchi hiyo. Lakini pia Raisi Kikwete alielezea jinsi gani Mwl. Nyerere alivyo
mpokea Mzee Mandela alipoondoka kwa siri kutoka Afrika kusini kuja Tanzania
bila kuwa na hati za kusafiria, lakini alipewa hati hizo na Tanzania na
kusafiri katika nchi za Ghana, Algeria na Ethiopia kama mtanzania. Raisi Kikwete
aliongelea pia uhusiano mzuri na wakaribu kati ya chama tawala cha Afrika
kusini ANC na chama tawala cha Tanzania CCM ulivyo imara. Raisi Kikwete alieleza jinsi gani watanzania
wameguswa na msiba huu wa Madiba na kusistiza kuwa tupo pamoja katika kipindi hichi kigumu cha msiba
wa Dunia nzima kwa ujumla.
TUNAKUPONGEZA RAISI
KIKWETE KWA KUIKUMBUSHA DUNIA JINSI GANI WATANZANIA TULIVYO WAKARIM NA JINSI
GANI TULIVYO NA UPENDO KWA MAJIRANI ZETU.
0 comments:
Post a Comment