MBOWE ATUMIA GARI LA KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI (SERIKALI) KATIKA MIKUTANO YA CHADEMA. Hizi ni picha halisi
Hili ni gari linalo tumiwa na
kiongozi mkuu wa upinzani Bungeni. Ni gari linalo milikiwa na serikali ya
Tanzania inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi kwa kutumia kodi halali za
wananchi wa vyama vyote. Chaajabu gari hili limeonekana katika shughuli za
kisiasa za CHADEMA katika mkutano uliofanyika maeneo ya Nyegezi Malimbe katika
viwanja vya shule ya msingi nyamalango na kuhudhuriwa na mwenyekiti wa chama
hicho taifa Bw. Freeman Mbowe kama msemaji mkuu wa mkutano huo. Nikitu kisicho
ruhusiwa kwa kiongozi yeyote wa serikali au chama chochote cha kisiasa kutumia
gari la serikali katika shughuri zozote
zile zinazohusu chama cha kisiasa. Ukweli ni kwamba kama jambo hili
lingefanywa na kiongozi wa chama kingine cha kisiasa kama CCM wanachama wa
upinzani hasa CHADEMA na viongozi wao wangelalamika na kuliita jambo hilo kuwa
ni matumizi mabaya ya mali za uma, lakini wao wameliona jambo hilo kama ni
halali. Jambo hili linaonekana kama ni moja ya ufisadi wa kichini chini
unaofanywa na kiongozi mkuu wa upinzani Bungeni kwa kushindwa kutumia gari za
chama chake katika shughuri zinazo husu siasa na chama chake badala yake
anaanza kutumia gari la serikali linalopaswa kutumika katika shughuri za
serikali tu.
0 comments:
Post a Comment