WASIRA NA NGEREJA WAWAFURAISHA WANAFUNZI WA SAUT. NIKATIKA KONGAMANO LA MIAKA 52 YA UHURU LILILOANDALIWA NA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU MKOA WA MWANZA.
Wageni waalikwa waliwasili mapema
saa 6 na nusu mchana. Wageni rasmi walikua ni M/kiti wa Chama Cha Mapinduzi
mkoa wa Mwanza Ndg. Antony Diaro, MNEC anaewakilisha wilaya ya Sengerema na Mbunge wa wilaya hiyo pia Ndg. William
Ngereja. Mgeni mwingine alikuwa ni Mb. Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Ndg. Steven
Wasira. Wakiambatana na wageni wengine
kama M/kiti wa UVCCM Ilemela Ndg.Kheri James, M/kiti wa UVCCM Nyamagana na
Wengine wengi.
Katibu mwenenezi wa tawi la
Kambarage SAUT aliwakaribisha wageni wote na kumkaribisha katibu wa CCM wilaya ya
Nyamagana ambaye naye alimkaribisha M/kiti wa tawi la kambarage kwaajiri ya
kumkaribisha Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza kwaajiri ya kumkaribisha M/kiti wa
CCM mkoa wa Mwanza Ndg. Antony Diaro kufungua kongamano rasmi naye alifanya
hivyo na kongamano lilianza kama ilivyokua imepangwa. Mgeni rasmi alitoa hotuba
nzuri naya kuvutia huku akikazia sana suara la watu kutokukubari kudanganywa na
watu wachache wanao potosha ukweli wa mambo. Baada ya hotuba mambo mengine
yaliendelea.
M/kiti wa tawi la Kambarage
alimkaribisha mtoa mada no.1 Ndg. Mwl. Julius Lugendo kwa ajiri ya kutoa na
kuielezea mada iliokua inahusu Harakati za ukombozi wa taifa letu kuanzia mwaka
1905 mpaka ukombozi ulipo patikana mwaka 1961. Mtoa mada huyo alihitimisha kwa
kusema ni lazima kila mtu ailinde na kuitunza amani tulionayo kwasababu ilipatikana
kwa gharama kubwa sana ilio husisha maisha ya watu wengi.
M/kiti wa tawi la Kambarage
alimkaribisha mtoa mada no.2 Ndg. Steven Wasira ambaye ni Waziri Ofisi ya Raisi
uratibu mahusiano na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM kwaajiri ya kutoa na kuielezea
mada aliyopangiwa. Mada hiyo ilikua inahusu Mstakabali wa serikali ya Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania na uwepo wa serikali tatu. Mh. Wasira alielezea vizuri
kuhusu mada hiyo hasa akikazia gharama ambazo Tanganyika itazipita baada ya
muundo huo wa serikali tatu. ‘‘ Tanganyika au Tanzania bara ndio itakayo beba
gharama zote za serikali tatu hizi kwa vile ndio inauchumi mkubwa na ina vyanzo
vingi vya mapato ukilinganisha na Zanzibar hivyo sio jambo zuri sana la
kuling’ang’ania kwa sababu lazima muungano wetu uliodumu kwa miaka 50
utavunjika kwa vile Tanganyika aitaweza kukubali kubeba gharama zote hizo’’
alisema Waziri Wasira pamoja na mambo mengie mengi. Mwisho Waziri Wasira
alisisitiza swala la uzalendo na kujijua miongoni mwa vijana wachapakazi wa
Tanzania.
Baada ya mtoa mada no.2 kumaliza
M/kiti wa tawi la Kambarage alimkaribisha mtoa mada no.3 Ndg. Peter Begga
amabaye alikuja kuelezea mada iliyokua inaeleza mafanikio ya taifa letu katika
Nyanja ya elimu. Ndg. Peter Begga alielezea vizuri kiwango cha elimu
kilichokuwepo wakati Tanganyika inapata uhuru na sasa. Wakati Tanzania inapata
uhuru ilikuwa na wanafunzi 14 tu wa chuo kikuu lakini sasa ni zaidi ya laki
moja na nusu. Peter Begga alimaliza kuongelea mada yake vizuri na kuzidi
kuwasisitiza wanafunzi wa chuo kikuu kufuata maadili ya kielimu na kuwa tofauti
na watu ambao hawajasoma ili kuwa mifano mizuri ya kuigwa.
M/kiti wa tawi la Kambarage
alimkaribisha Mbunge na MNEC anayewakilisha wilaya ya Sengerema Ndg. William
Ngereja ambaye alisimama kuielezea mada yake iliyokua inahusu Nafasi ya Vijana
katika ujenzi wa taifa. Mh. Ngereja alieleza kwa makini jinsi vijana wanavyo
pewa nafasi ya mbele na serikali yao kwa vile vijana ni zaidi ya 65% ya
wananchi wote watanzania. Mh. Ngeraja aliwataka vijana wote hasa wasomi wa vyuo
vikuu kutokukubali kutumiwa na Wanasiasa wasiokuwa na huruma na taifa lao.
Waziri huyo wa zamani wa Nishati na Madini alizidi kuwaomba vijana wazidi
kufanya kazi kwa nguvu zaidi ili wajikwamue kiuchumi na wanaosoma wazidi kusoma
sana ili kujenga taifa la wasomi hodari. Hivi ndivyo Mh. Ngereja alivyomaliza
kutoa na kuielezea mada yake.
Hivi ndivyo mambo
yalivyokuwa jana katika mahadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanzania
yaliofanyika jana katika ukumbi wa mwanza sekondari hapa jijini Mwanza
0 comments:
Post a Comment