MRISHO NGASA NI MIONGONI MWA MATUNDA BORA NA NYOTA YA ILEMELA. JE, UNATAKA KUWAJUA NA WENGINE NYOTA KAMA YEYE WANAO TOKA ILEMELA? ENDELEA KUTUFATILIA.
Mrisho Ngasa ni miongoni mwa
wanasoka bora na maarufu wa Tanzania anae iwakirisha vyema wilaya yake ya
Ilemela. Ni miongoni mwa wana soka wanao toka katika wilaya ya Ilemela.
Kiukweli wilaya yetu imekua miongoni mwa wilaya chache Tanzania zinazo zalisha
wachezaji bora Tanzania. Mrisho Ngasa
amekua mchezaji muhimu katika timu yetu ya taifa na pia katika virabu
mbalimbali ambavyo amefanikiwa kuvichezea hapa Tanzania. Virabu maarufu ambavyo
Mrisho Ngasa ameweza kuvichezea hapa nchini ni pamoja na Yanga SC, Simba SC, Azam
FC, Kagera Suger pamoja na TOTO
Africans. Kwa leo tumeona tukudokeze japo kidogo kuhusu huyu kijana wetu Mrisho
Ngasa ambaye katoka katika wilaya yetu safi na nzuri ya Ilemela. Sio yeye tu
wapo wachezaji wengi wanao toka katika wilaya ya Ilemela, tutazidi kuku julisha
mmoja baada ya mmoja. Endelea kutufatilia kila mara na kila muda ili uweze
kujua wachezaji hao zaidi. Sote kwa pamoja tunamuombea kwa Mungu azidi kumlinda na kumuinua zaidi na zaidi ili azidi kuitangaza vyema Wilaya yetu ya ILEMELA na Tanzania kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment