KATIBU WA CCM TAIFA NDG. ABDULRAHMAN KINANA AIKAMATILIA MBARALI.
Katibu mkuu wa Chama cha mapinduzi taifa Ndg.Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa wilaya ya Mbarali jijini Mbeya hapo jana. Katibu mkuu huyo ameambatana na katibu wa NEC itikadi na uenezi, na Dr. Asharose Migiro katibu wa NEC siasa na uhusiano wa kimataifa, katika ziara zake. Kinana ameelezea ujenzi wa barabara ambazo serikali yaelekea kuzijenga wilayani hapo, pia mchango wa serikali katika kilimo cha umwagiliaji kilichopo wilayani hapo Mbarali. Pia ndg. Abdulrahman Kinana amekuwa akikonga mioyo ya watanzania wengi, wakiwemo watu lukuki wanao rudisha kadi za vyama pinzani na kurejea nyumbani kwa watanzania wote walio wazalendo 'Chama Cha Mapinduzi'.
0 comments:
Post a Comment