MSHINDI WA EBSS, MWANZA KWA MARA NYINGINE YAZIDI KUNG'ARA YAZUA GUMZO KUBWA
Emmanuel Msuya kutoka ILEMELA Mwanza ndie mshindi wa Epiq
Bongo Star Search 2013
Mkurugenzi wa Bench Mark
Production na Chief Judge wa shindano la Epiq Bongo Star Search Madam
Ritha Paulsen (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Kampuni ya simu
za mkononi Zantel Bw. Ali Bakari kwa pamoja wakimkabidhi sanduku lenye
kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania Mshindi wa shindano hilo
Emmanuel Msuya ambae ni kijana kutoka Ilemela MWANZA. Mkoa wa MWANZA alimaarufu kama 'ROCKY CITY' unazidi kuibua vipaji mbalimbali nchini Tanzania, na hii ni mara ya pili kutoa mshindi wa BSS tangu mshindi wa BSS mwaka 2009 Pascal Casian. Shindano hilo ambalo ni chuo cha muziki kwa hapa nchini ambalo kwa sasa ni maalufu kwa jina la EBSS imetoa wanamuziki maalufu nchini na Afrika kama vile Peter Msechu, Pascal Casian ambae kwa sasa anafanya ziara mbalimbali za kimuziki barani Ulaya na Asia, Baby Madaha, Walter, Kala Jeremiah anae tamba na wimbo wake wa HIP POP uitwao Dear GOD, Jumanne Idi, Abubakhari Mzuri na wengine wengi. Mshindi wa EBSS 2013 Emmanuel Msuya amejinyakulia Tshs. 50,000,000/- taslimu.
0 comments:
Post a Comment