RAISI KIKWETE AZIDI KUTIMIZA AHADI ZAKE NA ZA CHAMA CHA MAPINDUZI
Rais Kikwete aendelea kutekeleza ahadi zake na ilani
za chama cha mapinduzi, azindua daraja la Mwanhuzi, mikoa mitatu kunufaika
AHADI ya ujenzi wa daraja la
Mwanhuzi wilayani Meatu, Simiyu imetimia baada ya Rais Jakaya Kikwete
kulifungua rasmi, baada ya ujenzi wake kukamilika na kuanza kutumika.
Kabla ya kulifungua daraja hilo,
Rais Kikwete aliwaasa wakazi wa Mwanhunzi na watumiaji wengine kulitunza daraja
hilo na kuhakikisha huduma ya usafiri kati ya Meatu na mikoa ya Arusha na
Singida inakuwepo.
“Ninawasihi mlitunze daraja hili na
asije akatokea mtu kwenda kuanza kukata vyuma au kunyofoa vifaa vingine vya
daraja, kwani kufanya hivyo mtadhohofisha ubora wake.
“Likiharibika kabisa tukajikuta
tunarudi kwenye kero ya usafiri wa eneo hili kama ilivyokuwa kabla ya kujengwa
daraja hili,” alisisitiza rais.
Daraja hilo lenye urefu wa mita 40
ni kiungo muhimu cha kuvuka Mto Mwanhuzi ilipo barabara kuu itokayo Kolandoto
mkoani Shinyanga kupitia Lalago mkoani Simiyu na kuelekea Singida na Arusha.
0 comments:
Post a Comment