KWAPAMOJA TUNAWEZA KUFANYA MAMBO YETU. MIAKA 52 YA UHURU MAFANIKIO NA MAENDELEO TUNAYAONA
Tunamshukuru Mungu wetu kwa alivyo tuunganisha kwa pamoja kusherekea miaka
yetu 52 ya uhuru wa taifa letu Tanzania pamoja na watanzania mlivyo jitoa
nakujitokeza kwa wingi. Hii inaonyesha jinsi gani watanzania bado mnaimani
kubwa na serikali yetu. Nijambo zuri kushirikiana kwa pamoja na kuweka tofauti
zetu mbali ili kufanya mabo yetu ya msingi kama hili la kusherekea miaka 52 ya
uhuru wetu. Hakika haya yote yanatokea na kufanyika ni kwasababu ya serikali
nzuri iliyopo madarakani inayo ongozwa naz Chama Cha Mapinduzi, inayotuunganisha
pamoja bila kubaguana kwa dini na kabila zetu. Wapo wenzetu wengi wanao tamani
kuhishi kama sisi watanzania tunavyoishi lakini wameshindwa kwa vile tu
hawaishi kwa amani kama tulionayo sisi. Tuilinde na kuitunza amani yetu.
0 comments:
Post a Comment