MAELFU WAJITOKEZA KUMLAKI SHUJAA WAO ZITTO KABWE MKOANI KIGOMA. WAPIGA KULA WAKE WAMLAKI KWA MABANGO YA USHUJAA NA USEMA KWELI. CHADEMA WADUWAA!
Hivi ndivyo mapokizi ya Zitto Zuberi Kabwe yalivyo fanyika mapema leo
mkoani Kigoma. Mapokezi haya yanahashiria kuwa wapiga kula wa Zitto Kabwe
hawapo pamoja na viongozi wa wa juu walioafikiana kumvua madaraka Naibu Katibu
mkuu huyo wa wa zamani wa CHADEMA siku kadhaa zilizopita. Maelfu ya watu
wakiwemo wafuasi wa CHADEMA na vyama vingine vya Siasa wamejitokeza kumlaki kwa
nderemo na vifijo mbunge na shujaa wao huku wakiwa wamebeba mabango
yalioandikwa maneno tofauti tofati huku wakiashiria kumpongeza na kumtia moyo
kiongozi wao huyo. Kwa namna moja au nyigine wanakigoma hao na wafuasi wa Zitto
Kabwe wanadhidi kuonyesha kuwa wapo pamoja nae ata kama atafukuzwa na chama
chake na kujiunga na chama kingine.
Wana siasa wengi wa Tanzania
wanadhani watanzania bado niwajinga kama ilivyokuwa miaka kadhaa iliyopita na
kumbe watanzania waliisha amka zamani na hawapo tayari kuburuzwa kama wajinga
tena.
Kwa hili tunawapongeza sana
wapiga kula wa Zitto Kabwe kwa ujasili na mshikamano mnao onyesha kwa kiongozi
wenu mwadilifu na msema kweli na nyinyi ndio mliosababisha CHADEMA wakamtambua
Zitto Kabwe kama ni miongoni mwa wabunge wake.
MUNGU AWATANGULIE
WANA KIGOMA KWANI HUYO NDIO KIONGOZI
WENU MLIOMCHAGUA KWA KULA ZENU NA SIO KWA KULA ZA UKOO WA…………………………………
0 comments:
Post a Comment