SARAFU MOJA AFRIKA MASHARIKI YAANZISHWA, TANZANIA KUNUFAIKA
Jana viongozi wa nchi wana chama wa jumuia ya Afrika Mashariki walikubaliana kuanzisha matumizi ya sarafu moja kwa nchi wanachama wa jumuia hiyo. Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, raisi wa jamuhuri ya Kenya mh. Uhuru Kenyatta, raisi wa jamuhuri ya Burundi mh.Pierre Nkrunziza, raisi wa jamuhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni pamoja na raisi wa jamuhuri ya Rwanda Paul Kagame wote kwa pamoja walikubaliana kwa pamoja na wakasini kuanzisha sarafu moja ya jumuia ya nchi hizi. Sarafu hiyo ya jumuia ya Afrika Mashariki (EAMU)-East African Monetary Union. Kuanzishwa kwa sarafu moja ya nchi za Afrika Mashariki kutainufaisha Tanzania kiuchumi? Hili swali ni lamsingi kwa maendeleo ya uchumi wa nchi yetu na kwa maendeleo ya watanzania wote kwa ujumla. Kazi imebaki kwatu sisi watanzania kuhakikisha tuna fanya kila njia kuakikisha uchumi wetu unastawi zaidi.
0 comments:
Post a Comment