WAAFRIKA KUSINI WAIBARIKI TANZANIA. NI BAADA YA KUGUNDUA UKOMBOZI WAO ULIANZIA TANZANIA. WENGI WALIKUA HAWAJUI. WAMKUMBUKA TENA NYERERE.
UHUSIANO
baina ya Tanzania na Nelson Madela ulichochewa na mauaji ya Sharpeville
yaliyotokea mwaka 1960; na ulipita katika majaribu mengi yakiwamo mkutano baina
ya Madiba na Mwalimu Nyerere mwaka 1962.
Mapitio
ya maandishi mbalimbali pamoja na mahojiano ambayo gazeti hili limefanya na
watu waliofahamu uhusiano baina ya Mandela, Nyerere, nchi pamoja na vyama vyao,
yameeleza mengi kuhusu uhusiano huo wa kihistoria baina ya nchi hizi.
Maandishi
katika mtandao wa chama tawala cha ANC cha Afrika Kusini, yanaonyesha namna
uongozi wa juu wa chama hicho ulipoamua kuhamia Tanganyika baada ya serikali
dhalimu ya makaburu wa Afrika Kusini kukipiga marufuku chama hicho pamoja na
kile cha PAC, baada ya mauaji hayo ya Sharpeville.
Chama
hicho kilimtuma kada wake, Frene Ginwala, kuja nchini hapa mwaka huo huo wa
1960 na yeye ndiyo hatimaye aliyepanga mipango ya kuwasafirisha kwa siri
viongozi wa juu wa ANC kama vile Oliver Tambo na Yusuf Dadoo kuja Tanganyika
wakati huo.
Baadaye,
Ginwala alipewa kazi na Mwalimu Nyerere kama mhariri wa gazeti la serikali la
Standard (sasa Daily News) na Baba wa Taifa ndiye aliyewapokea akina Tambo na
huo ndiyo ukawa mwanzo wa uhusiano wa kipekee baina ya Tanzania na wapigania
uhuru wa Afrika Kusini.
Chama
cha ANC kinasema kwamba wakati chama hicho kilipoamua kutumia nguvu kuung’oa
utawala wa makaburu, kilimtuma Mandela kuja Tanganyika ili kuzungumza na
Nyerere kwa ajili ya kupewa msaada wa kifedha na mafunzo.
“Hata
hivyo, mkutano huo wa kwanza baina ya Nyerere na Mandela haukuisha vizuri kwa
sababu Mwalimu aliwataka ANC kusitisha njia ya mapigano hadi kwanza utawala wa
makaburu utakapomtoa gerezani mpigania uhuru mwingine wa chama cha PAC, Robert
Sobukwe.
“Nyerere
pia alikuwa na uhusiano mzuri na Sobukwe na kwa kweli Mandela hakufurahishwa
sana na ushauri huo wa Nyerere. Hata hivyo, katika miaka iliyofuata uhusiano
huo, Tanzania ilikuja kuwa mshirika mzuri sana wa ANC,” unasema mtandao wa
www.sahistory.org.za
Taarifa
rasmi zinaeleza kwamba Tanzania ndiyo yalikuwa makao makuu ya kwanza ya ANC na
PAC na hadi kufikia mwaka 1965, jumla ya wapigania uhuru 800 walikuwa wanapata
mafunzo katika vyuo vya Mazimbu, mkoani Morogoro na Kongwa mkoani Dodoma.
Mazimbu
na Kongwa
Nyerere,
baadeye kubali kuanzishwa kwa kambi ya kwanza ya mafunzo ya kijeshi ya
wapiganaji wa kundi la Umkhonto wa Sizwe wilayani Kongwa mkoani Dodoma kati ya
mwaka 1963 na 1964 na serikali ya Tanzania ilikuwa ikigharamia sare na mlo
mmoja wa wapiganaji hao.
Miongoni
mwa walioanzisha kambi hiyo ni Joe Modise ambaye baadaye alifikia kuwa Waziri
wa Ulinzi katika serikali isiyokuwa ya kibaguzi ya Afrika Kusini.
Kambi
ya Mazimbu ndiyo ambayo baadaye ilikuja kujenga chuo cha mafunzo maarufu kwa
jina la Solomon Mahlangu (SOMAFCO).
Maelezo
mbalimbali yanaonyesha kwamba aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Moroagoro katika miaka
ya 1970, Anna Abdallah (baadaye alikuja kuwa waziri katika wizara mbalimbali na
sasa mbunge), ndiye aliyewapa eneo hilo wapiganaji hao wa ANC.
Nusura
uhusiano uvunjike
Mwaka
1969, uhusiano baina ya ANC na Tanzania ulifikia katika hatua mbaya. Kada wa
TANU, Oscar Salathiel Kambona, alidaiwa kutaka kumpindua Nyerere kwa kushirikiana
na wapiganaji wa Umkhonto waliokuwa wamechoka kufanya mazoezi hapa nchini
pasipo kutumwa kurudi kwao kuanzisha mapambano.
Maelezo
kuhusu hilo yalitolewa na kada wa PAC, Potlako K. Lebalo, na serikali ya TANU
iliamua kurejesha makambini wapiganaji wote wa ANC waliokuwepo ikiwa ni pamoja
na kukiondoa chama hicho hapa nchini.
Hata
hivyo, mwana historia wa ANC, William Gumede, anasimulia kwamba Tambo aligoma
kulazimishwa kwa wapiganaji hao kufungiwa makambini; kwa maelezo kwamba wao ni
“Wapigania Uhuru na si wakimbizi.”
Huo
ndiyo ukawa mwanzo wa ANC kuhamishia Lusaka makao yake makuu ambayo yalidumu
hadi chama hicho kiliporuhusiwa tena kushiriki katika siasa.
Hata
hivyo, serikali ya Tanzania ilikuwa na msimamo mkali pia dhidi ya wanachama wa
ANC waliokuwa na mrengo wa kikomunisti. Hiyo ndiyo sababu wanachama kama
Michael Harmel, Dadoo, Joe Slovo na Ruth First baadaye walipigwa marufuku
kukanyaga katika ardhi ya nchi hii.
Hata
hivyo, kutokana na mauaji ya Soweto ya mwaka 1976, ambayo pia yalisababisha
utawala wa makaburu kukamata watu wengi zaidi, ndipo wananchi wengine
wakakimbia Afrika Kusini na kuja Tanzania.
Hapo
tena, Anna Abdallah, kwa maelekezo ya Nyerere, alitafuta eneo katika mkoa wake
kule Dakawa ambako nako ikawa kambi ya wapiganaji.
Alipotoka
jela, Mandela kwanza alitembelea Lusaka yalikokuwa makao makuu ya ANC na ndipo
akafanya ziara yake ya kwanza nchini Tanzania ambapo alipokewa na Mwalimu
aliyekuwa amestaafu tayari.
HEKIMA NA BUSARA ZA BABA YETU NYERERE ZITATUTANGAZA VEMA MPAKA MWISHO WA DUNIA.
0 comments:
Post a Comment